PICHA ZA UKWELI

GAZETI LA Mwana Halisi LAFUNGIWA


SERIKALI ya Jamhuri ya Tanzania, imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwakile kilichoelezwa kuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchozezi.
Sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi. 
Akisoma tamko la Serikali leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
“Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii,pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari”alisema
Aidha alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
“Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulika kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i),adhabu hiyo itaanza tarehe 30 julai,2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dra es salaam julai 27,2012”alisema
chanzo:-http://sufianimafoto.blogspot.com/

CCM,Chadema wawatangazia kiama wabunge mafisadi


 
Mkutano ukiendelea Bungeni
DK SLAA AONYA HAKUNA HURUMA, MSEKWA ASEMA RUSHWA  ADUI WA HAKI, MBATIA ATOA WIKI MOJA SPIKA AWATAJE WOTE   
Kizitto Noya, Dodoma na Leon Bahati, Dar
VYAMA vya CCM na Chadema vimetoa onyo kali kwa wabunge wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuhongwa na baadhi ya kampuni za mafuta na kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vikisema havitasita kuwawajibisha pindi tuhuma hizo zitakapothibitika.
Kauli ya vyama hivyo imekuja siku moja baada ya wabunge watano, watatu wa CCM na wawili wa upinzani kudaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa, ambavyo vimesababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili majina ya wahusika yawekwe hadharani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa juu wa vyama hivyo walisema wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka bungeni.
CCM: Rushwa adui wa haki
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema chama hicho kimewaapiza wanachama wake wote kutotoa wala kupokea rushwa.

Alisema rushwa ni kosa la jinai hivyo anaamini vyombo husika vya dola vitachukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikazia kauli hiyo akisema rushwa inaelezwa katika katiba ya chama hicho kwamba ni, ‘adui wa haki’ na wanachama wote waliapishwa kuwa hawatapokea wala kutoa rushwa.
Alisema yeyote anayekwenda kinyume na kanuni za CCM, anajiweka katika kundi la wasaliti wa chama.

Alisema wabunge ni kundi maalumu nchini ambalo linalipwa vizuri ili lisimamie vyema misingi ya maendeleo ya nchi pasipo tamaa wala vishawishi hivyo wanapotajwa miongoni mwa kundi la wala rushwa, CCM kinalaani vikali tukio hilo.
Kuhusu tuhuma hizo kutajwa kuwahusisha wabunge watatu wa chama hicho, Nape aligoma akisema habari hizo siyo rasmi, hivyo hawezi kuzizungumzia.
Hata hivyo, alisema CCM kinasubiri uchunguzi ufanyike ambao  ndiyo utakaoweka bayana wahusika wa tuhuma... “Tusubiri uchunguzi ukamilike.  Idadi inawezekana ikawa hiyo au ikapungua au kuongezeka.”

Dk Slaa: Hatufumbii macho ufisadi
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: “Nalaani kitendo cha wabunge kuhusishwa na ufisadi hasa ikizingatiwa kwamba Chadema tumekuwa tukiupinga vikali. Tumekuwa tukipinga rushwa kwa sababu ndiyo inayoielekeza nchi pabaya… Chadema hatufumbii macho rushwa.”

Alisema tangu kuanza Bunge la 10, Chadema kimekuwa kikiona baadhi ya mambo yanayoendelea katika mhimili huo muhimu wa dola yamejaa walakini... “Ndiyo maana sisi Chadema tumekuwa tukisema Bunge limepoteza mwelekeo.”
Alisema akiwa mtendaji mkuu wa chama, anasubiri taarifa kamili kutoka katika kikao cha wabunge wa chama hicho ili kuweka wazi majina ya wahusika na kisha kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu (CC) ambacho kitakaa na kuchukua hatua kali.
“Tunahitaji tupate maelezo ya kina... chama chetu hakikurupuki… Nasubiri taarifa ya kokasi ya chama. Katiba ya Chadema inatambua uwapo wa kikao cha wabunge wetu na kwa bahati nzuri, kiongozi wake mkuu ni Mwenyekiti wa Chadema (Freeman Mbowe) na katibu (David) Silinde ni mbunge wetu. Tunasubiri taarifa yao.”
Alisema Chadema kina kanuni ya kudhibiti rushwa hivyo, mbunge wake akitajwa miongoni mwa wanaohusishwa na rushwa, atawajibishwa kupitia kikao cha CC ya chama hicho.
NCCR-Mageuzi  yakoleza moto

Katika hatua nyingine, Chama cha NCCR- Mageuzi jana kilikoleza moto baada ya kumtaka Spika Anne Makinda awataje wabunge hao bungeni ili wafukuzwe na kufungwa kama Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inavyotaka.

Chama hicho kimetoa wiki moja kwa Spika Makinda kufanya hivyo, kikionya kuwa vinginevyo, chenyewe kitawasilisha hoja mahususi kutaka Bunge lichukue hatua hiyo.
Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alitoa tamko hilo mjini Dodoma, akisema  Sheria Namba 3 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988, inataka wabunge wanaothibitika kujihusisha na rushwa wafukuzwe na kufungiwa kwa kipindi cha miaka mitano.
“Ni aibu kwa Bunge, taasisi inayoitwa tukufu kuwa na mafisadi. Kitendo cha Spika kukubali kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na kuahidi kuzivunja nyingine, maana yake anakubali kuna mafisadi. Sisi tunamtaka atutajie wabunge hao bungeni ndani ya juma moja,” alisema Mbatia.
Mbatia aliyeongozana kwenye mkutano huo na wabunge Moses Machali wa Kasulu Mjini na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini), alisema pamoja na Bunge kuendeshwa kwa kanuni zake, kwa Tanzania kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola inaweza pia kuiga yaliyofanywa katika nchi nyingine za jumuiya hiyo, zikiwamo India na  Uingereza.
Kwa mujibu wa Sheria zinazotumika katika nchi hizo, mbunge yeyote anayethibitika kutumwa na mtu nje ya Bunge, kuongea au kuandika bungeni kwa masilahi ya mtu huyo, anapaswa kufukuzwa ubunge na kufungwa.
“Kati ya mwaka 1924 na 1956, Uingereza ilifukuza wabunge 59 na kati ya mwaka 2005 hadi sasa, Bunge la India liliwafukuza wabunge 11 baada ya kuthibitika walihongwa na wafanyabiashara kuuliza maswali binafsi,” alisema.
Mbatia aliendelea kueleza kuwa katika Bunge la Nane nchini, wabunge wanne walikamatwa na kushtakiwa, kisha chama chao CUF, kiliwazuia kujihusisha tena na siasa baada ya kubainika kuwa walifunga ndoa batili na Wasomali ili wapate hati ya kuishi nchini.
“Sasa suala hili, wabunge wote wanaohisi wamo kwenye orodha hii ya ufisadi waachie ngazi. Mbunge yeyote na wa chama chochote anayeona ameshiriki uchafu huu, kwa utashi wake aachie ngazi,” alisema na kuongeza:
“Kwa vile vyama viadilifu, waige mfano wa CUF. Bunge lichukue nafasi yake kabla hatujafunga Bunge Agosti 18 tuwe tumefanya uamuzi wa kuwafukuza.”

Mbatia alisema ili Bunge lilirudi kwenye heshima yake, Spika Makinda pia anapaswa kuzitaja kamati nyingine alizosema zinachunguzwa na ikiwezekana nazo zivunjwe ili haki itendeke.
“Sisi (NCCR-Mageuzi) tunataka pia Spika azitaje kamati hizo, ziko sita na tuseme pia kwamba hatuna imani na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge. Tunataka nayo ijisafishe kwanza kwa kuwa nako kuna watuhumiwa.”
“Katika hili niombe kiti cha Spika kitende haki, hata kama kuna mbunge wa NCCR-Mageuzi anahisi alishiriki ufisadi huu, awahi mapema kuondoka, hii isiwe kwa vyama vingine tu,” alisema.

Mbatia alisema suala la Tanesco ni tone tu, akisema ufisadi kwa wabunge ulianza siku nyingi na kuongeza... “Mheshimiwa Kafulila (David) aliwataja wajumbe wa Kamati ya LAAC lakini, mpaka leo hakuna kinachoendelea.”
Alisema tatizo la ufisadi kuhusisha wabunge lilianza Juni 23, 2006 siku ambayo nchi iliingia mkataba na Kampuni ya Richmond... “Kuanzia hapo kumeendelea kuwa na sintofahamu katika Wizara ya Nishati na Madini. Dawa yake ni kuweka mikakati ya Bunge kujitakasa.”

Sakata lenyewe

Wabunge hao watano (majina tunayahifadhi kwa sasa) wanatuhumiwa kutumia nafasi zao za uwakilishi bungeni au ujumbe ndani ya kamati husika, kufanya biashara na Tanesco na kutetea mafisadi wanaolihujumu shirika hilo kutoka ndani na nje.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliochangia hoja hiyo bungeni walisema wanawafahamu wabunge hao kwa majina, lakini wasingependa kuwataja kwa kuwa siyo wakati mwafaka.
Moto wa kutaka kutajwa kwa majina ya wabunge hao ulikolezwa na Mbunge wa Namtumbo (CCM),
Vita Kawawa  ambaye aliomba Spika avunje Kamati ya Nishati na kutaka pia Bunge lijadili kashfa hiyo.

“Waheshimiwa wabunge wamejadili suala hili kwenye wizara, lakini kwa mujibu wa Kifungu cha 55 (3) f, Mbunge au Waziri anaweza kutoa hoja ili jambo fulani lijadiliwe.
Sasa mimi naomba kutoa hoja ya kujadili suala hilo.”Baada ya hoja hiyo kuungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge , ndipo Spika Makinda aliposimama na kukubali hoja hiyo ya Mbunge Vita Kawawa na kutangaza kuivunja kamati hiyo.
Spika Makinda alisema tayari pia, ameagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia hiyo ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.
“Nasema kwa dhati kabisa kitendo hiki hakikubaliki ndani ya Bunge. Wabunge mkae vizuri, kama kuna baadhi yetu wanakwenda huku na huku kujitafutia masilahi binafsi mnawezaje kuisimamia Serikali?”

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Seleman Zedi alisema ameshtushwa na uamuzi huo wa Spika na kwamba anasubiri uamuzi wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Akihitimisha hoja ya wizara yake bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema baadhi ya wabunge ambao wanashiriki kwenye vikao vya uamuzi vya Tanesco kama wajumbe wamekuwa wakilihujumu shirika hilo kwa njia mbalimbali ikiwamo kufanya nalo biashara.
“Shirika liliwahi kulipa Paundi 50,000 za Uingereza kwa ajili ya ununuzi wa vipuri, lakini kilicholetwa nchini ni masanduku ya misumari. Nguzo hizo za umeme kuna biashara inaendelea. Tunajua kwamba nguzo hizo zinazalishwa Iringa na kupelekwa Mombasa kisha kurudishwa nchini kwa maelezo kwamba zimetoka Afrika Kusini,” alisema Profesa Muhongo

TUSUBURI TUMUONE HUYU JAMAA-HUSSEIN BOLT


Usain Bolt 

















Ah, the Olympics. That special event that comes around every few years to warm our hearts, chill our spines, and remind us that we're really not as good at things as other people. Over the years, there have been some very talented people treating the world to some very exciting, inspiring, and memorable moments. From underdog victories, to heart-warming testaments of humanity, the Olympics have given the world some pretty damn good TV.

Hollywood.com has compiled a gallery of the 10 Most Exciting Olympic Moments in celebration of the 2012 Summer Olympics, which is bound to grant us the same unforgettable twists of fate as years past. Click the link below to check out the gallery, and sound off about your favorite Olympic moments in the comments section!

BENFICA Vs REAL MADRID-FRIENDLY MATCH


Benfica 5-2 Real Madrid footyroom.com (2) by Futbol2101

KAMANDA AKIWAJIBIKA-LEO JUMATATU


Rais Dkt.Jakaya Kikwete amjulia hali bibi kikongwe(85) katika kijiji cha Msoga


 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki  jana (Jumapili).(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki jana(Jumapili).(picha na Freddy Maro).

London 2012 Olympics: Vasilii Belous (Moldova) crushes Selemani Kidunda (Tanzania)

Moldova's Vasilii Belous has kicked off the Olympic welterweight competition with a crushing victory over Selemani Kidunda of Tanzania


Belous took the bout at his own pace, landing plenty of scoring punches in the first round to establish a six-point lead.

The Moldovan extended his lead by two points, before a devastating final round that saw him stun the Tanzanian with a speedy left-right combination.

The judges confirmed Belous's superiority with a 20-7 scoreline. 
Picture
Tanzania's Selemani Kidunda (R) fights against Moldova's Vasilii Belous in the men's welter (69kg) Round of 32 boxing match at ExCeL venue during the London 2012 Olympic Games July 29, 2012. REUTERS/Murad Sezer (BRITAIN)
Lightweight (132 lbs/60kg)

8:30 a.m. - Wellington Arias (Dominican Republic) vs Eduar Marriaga (Colombia)
Winner will face Vasyl Lomachenko (Ukraine), who has a bye.

8:45 a.m. - Ahmed Mejri (Tunisia) vs Shafiq Chitou (Benin)
9:00 a.m. - Felix Verdejo Sanchez (Puerto Rico) vs Juan Huertas Garcia (Panama)

9:15 a.m. - Gani Zhailauov (Kazkhstan) vs Saylom Ardee (Thailand)
9:30 a.m. - Andrique Allisop (Seychelles) vs Jai Bhagwan (India)

9:45 a.m. - Luke Jackson (Australia) vs Qiang Liu (China)
Winner will face Yasnier Toledo Lopez (Cuba), who has a bye.

Welterweight (152 lbs/69kg)

10:00 a.m. - Selemani Kidunda (Tanzania) vs Vasilii Belous (Moldova)
Winner will face Taras Shelestyuk (Ukraine), who has a bye.

10:15 a.m. - Tuvshinbat Byamba (Mongolia) vs Yannick Mitoumba Mbemy (Gabon)
10:30 a.m. - Alexis Vastine (France) vs Patrick Wojcicki (Germany)

10:45 a.m. - Custio Clayton (Canada) vs Oscar Molina Casillas (Mexico)
11:00 a.m. - Moustapha Abdoulaye Hima (Niger) vs Cameron Hammond (Australia)

11:15 a.m. - Freddie Evans (Great Britain) vs Ilyas Abbadi (Algeria)
Winner will face Egidijus Kavaliauskas (Lithuania), who has a bye.

MHE JOHN KOMBA AREJEA BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI INDIA


Kampteni Komba akiwa na mkewe, Salome Komba nyumbani kwako Kawe, jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni mstaafu, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa kulia.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo, Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi, Kawe, Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini, Juzi, baada ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.
Alisema, aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.
"Siku napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda kutibiwa nje", alisema Komba.
Alisema, uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo 138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.
"Amesema, baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata hivyo ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo atalazimika kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba mwaka huu kama alivyoelekezwa na madaktari.
Akizungumzia upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na kukamilika bila matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu iliyopasuliwa ni ya ukumbwa wa futi moja.
Alisema, hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya kawaida, kwa sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha, hivyo akalazimika kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) kwa siku tano.
"Sasa nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo kabisa", alisema Komba.
Komba alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika kuugua kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.
"Jamani ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika siyo kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika eti naugua figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu lingepata kwa uhakika ninachoumwa", alisema Komba.

PICHA ZA UKWELI ZA LEO

Mwanamuziki JOSE CHAMELEONE Afanya Maandamano Ubalozi Tanzania nchini Uganda Kushinikiza Arejeshewe Paspoti Yake.

Mwanamuziki Jose Chameleone akiimba nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Uganda
Baadhi ya watu mablimbali walioungana na Mwanamuziki Jose Chameleone
 Gari la Polisi likiwa nje ya Ubalozi Tanzania nchini Uganda
Mwanamuziki mashuhuri nchini Uganda Jose Chameleone akiwa nje ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda na mabango sambamba na wapambe wake akishinikiza apatiwe passport yake ambayo anadai inashikiliwa na Bwa.Erick Shigongo.Picha mbalimbali kama zinavyoonesha tukio hilo nje ya jengo la Ubalozi Tanzania nchini Uganda.Picha zaidi ingia kwenye www.facebook.com/josechameleone

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjamin Mkapa Awasili Mkoani Songea


  Kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Joseph Mkirikiti akimkaribisha  Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjamin Mkapa katika uwanja wa ndege wa Songea.
  Meya wa manispaa ya Songea mstahiki Charles Mhagama  akisamiana na rais mstaafu wa awamu wa tatu Mhe Benjamin Mkapas baada ya kutua  mjini Songea
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Joseph Mkirikiti kushoto akimuongoza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjamin Mkapa kwenda kuangalia vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege mjini Songea.
Rais wa awamu ya tatu Mhe Benjamin Mkapa  akiangalia vikundi vya ngoma (havipo pichani)  katika uwanja wa ndege wa Songea akiwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe Joseph Mkirikiti. Katikati ni mwenyekiti wa CCM  mkoa Cornel Msuha kulia ni mama Anna Mkapa na wa pili kulia mke wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu Mama Afisa Mwambungu.

KUMEKUCHA TAMASHA LA “CHAGGA DAY CULTURAL FESTIVAL 2012”

BENDI  zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
Akizungumza na waandishi wa habari  mapema jana ukumbi wa Udara habari Maelezo, ijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul  Maganga walioandaa tamasha hilo lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema  Maganga
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua mila zao  sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa  kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya  makabila mbalimbali  nchini Tanzania.
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata kujua chimbuko la kuweko kwa  tamaduni zao  yaani mashujaa wa makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.
Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro,  SBC Tanzania (Pepsi), Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili Restaurant, Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel &Tours, Dotnata Decorations.

MASUDI LEO





For sleeping with another man's wife, this was his reward


Pouring acid on one another was known as a woman’s game but for the case of Emmanuel Byaruhanga, 34, the tables were turned.

Emmanuel, a business man who deals in buying and selling of food, Matooke in particular is said to have got another man’s wife pregnant and in revenge, the husband of the woman poured acid on him which destroyed his physical assets.

He was taken to Mulago hospital after he met with his fate. Narrating his story, Emmanuel said between 8:00pm and 8:30pm, as he was watching a movie with his friends, one of his friends, Muchunguzi who is commonly known as Katogo, a tailor asked people sitting next to him to leave and sit aside but a few refused to heed to his request and they got burned as Emmanuel.

They were watching the movie from a local cinema commonly known as ‘kibanda’ and the owner of the place, is one of the suspects according to Emmanuel. He said the mother of his child had actually separated from the husband when they got together and later on became pregnant.

The owner of the local cinema was husband to the woman whom Emmanuel impregnated and later on gave birth; she informed him about what had happened to him something which clearly did not please him.

The woman in dispute, Florence Nakirijja informed reporters that she had just called the Emmanuel to tell him to buy books for the children before the shops had been closed only to receive another phone call saying he had been injured. She is currently with him at hospital taking care of him.

The incident took place in a village called Jjaga Kabuyoga in Lwengo district.

 Mirembe Martina via UgandaPicks.com