SERIKALI
ya Jamhuri ya Tanzania, imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda
usiojulikana kwakile kilichoelezwa kuwa na mwenendo wa kuandika habari
na makala za uchozezi.
Sababu
nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na
uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya
dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi.
Akisoma
tamko la Serikali leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya
Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti
hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia
yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
“Mhariri
wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki
kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii,pia hazifuati
weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari”alisema
Aidha
alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa
akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa
maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo
kinachoweka ukomo wa uhuru.
“Serikali
imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulika kwa
mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i),adhabu
hiyo itaanza tarehe 30 julai,2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali
namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini
Dra es salaam julai 27,2012”alisema
chanzo:-http://sufianimafoto.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment