BENDI  zenye ushindani
mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina
yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja
vya Leaders.
Akizungumza na waandishi wa habari  mapema jana ukumbi wa Udara habari Maelezo, ijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul  Maganga walioandaa tamasha hilo
lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi,
alisema  siku hiyo itakua ya aina yake
kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja
tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki
tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya
utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na
makabila mengine  na burudani kutoka kwa
bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja
na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema  Maganga
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la
wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu,
ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na
vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema 
baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine
litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe
mbalimbali
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha
haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua
mila zao  sambamba na kudumisha utamaduni
wa Mtanzania kwa  kuwakumbusha tamaduni
zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya  makabila mbalimbali  nchini Tanzania.
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo,
watapata kujua chimbuko la kuweko kwa 
tamaduni zao  yaani mashujaa wa
makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.
Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni
pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro,  SBC Tanzania (Pepsi), Dstv,Homeshopping
Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC Africa,Giraffe Hotel,BM
barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili Restaurant, Auckland Safaris
&Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel &Tours, Dotnata Decorations.
No comments:
Post a Comment