WATU watatu wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa kutokana na
ajali ya gari iliyo itokea maeneo ya Burka bara bara ya dodoma
–Arusha baada ya gari aina ya Toyota hiace lenye namba za usajili T
706 kugongana na gari aina ya Toyota hilux lenye namba za usajili T
509 AJW ukio hilo lililokuwa likitokea mjini kuelekea kisongo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo limetokea mnamo july 15 majira
ya saa sita mchana.
Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea wakati gari aina ya Toyota hiace
kujaribu kulipita gari aina ya landrover iki katika ajambayo ni mali
ya Leopad Tours ambalo lilikuwa mbele yake hivyo kusababisha hadi
kutokea kwa tukio hilo.
Aidha Kamanda Sabas aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni
Hassan Twaha ambayue ni kondakata wa Haice na mkazi wa mbauda
,mwingine ni Dachu aliyetambulika kwa jina m0ja tu na ambaye makazi
yake hayakujulikana na marehemu wa tatu ni ,mwanamke ambaye hakuweza
kufahamika mara moja.
Alieleza kuwa waliojeruhiwa ni kumi na tatu ambapo watano kati yao
wamelezwa katika hospitali za hapa mjini na kwamba hali zao
zinaendelea vizuri na tayari wanane kati yao wametibiwa na kuruhusiwa
kurudi majumbani.
Aliwataja waliolazwa kuwa ni pamoja na askari magereza mwenye namba B
1952 CPL Hussein Ally mkazi wa kisongo,Mohamed Juma,Festo Damas ambaye
ni dereva wa boda boda ,Jabir Abrahamu ambaye ni kondakta wa hiace
.
Mwingine ni bw Robert Wilbert( 32) ambaye ni dereva wa Hiace ambaye
naye amelazawa katika hospitali ya selian na mpaka sasa yupo chini ya
ulinzi wa jeshi la polisi kujibu tuhuma za kusababisha ajali hiyo
No comments:
Post a Comment