Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya
MAN UNTIED YAKWAMA KWA MOURA
KLABU ya Manchester United imefeli jaribio la kumnasa kiungo wa
Sao Paulo ya Brazil, Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, kwa dau la
pauni Milioni 29.8, kwa mujibu wa klabu hiyo ya Brazil.
KIUNGO Oscar, mwenye umri wa miaka 20, amewasili London na kikosi cha
Brazil cha Olimpiki na atafanyiwa vipimo vya afya kuelekea kusajiliw
akwa dau la pauni Milioni 25, akitokea klabu ya Internacional kwenda
Chelsea.
MSHAMBULIAJI Dimitar Berbatov anaweza kujiunga na AC Milan au
Juventus, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo wa Manchester United.
KOCHA mpya wa Watford, Gianfranco Zola anamtaka gwiji wa Italia, Filippo
Inzaghi, mwenye umri wa miaka 38, na Alessandro Del Piero, mwenye miaka
37, ambao wote kwa sasa ni wachezaji huru.
KLABU ya Barcelona inaweza kumfuata beki wa Liverpool, Daniel
Agger baada ya kumkosa kiungo wa Athletic Bilbao, Javi Martinez, mwenye
umri wa miaka 23.
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa, Bafetimbi Gomis, mwenye umri wa miaka 26, ataachana na mpango wa kuhamia wa Tottenham, ili abaki Lyon.
MSHAMBULIAJI Robin van Persie anajiandaa kwa mazungumzo na kocha
wa Arsenal, Arsene Wenger katika msistizo wa kuondoka The Gunners.
Mshambuliaji huyo wa Uholanzi, mwenye umri wa miaka 28, ameonyesha nia
ya kujiunga na Juventus au Manchester United.
KLABU ya Fulham imeanza mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 19.
BEKI wa Manchester City, Kolo Toure anaweza kujiuza mwenyewe kwa
klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia, ambako atakuwa akipata mshahara wa
pauni 50,000 kwa wiki, hiyo ikiwa nje ya kodi na nyumba ya kuishi pamoja
na gari mbili atakazopewa, kulipiwa tiketi za ndege na huduma nyingine.
KOCHA wa Sunderland, Martin O'Neill anataka kurejea klabu yake ya
zamani, Aston Villa kumsajili James Collins. Villa inajiandaa kumuuza
nyota huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 28, huku wakiwa karibu kumnasa
Mholanzi wa Feyenoord,l Ron Vlaar, mwenye umri wa miaka 27.
KLABU za Everton na West Brom inataka kumsajili beki wa FC
Copenhage, raia wa Costa Rica, Bryan Oviedo, mwenye umri wa miaka 22,
ambaye amekuwa akifuatiliwa na Manchester United pia.
BEKI Scott Dann anaweza kujiunga na Ajax kwa mkopo kufuatia kushuka
daraja kwa Blackburn. Reading na Southampton zimefeli kumsajili beki
huyo anayeuzwa pauni Milioni 6.
KIUNGO wa Tottenham, Danny Rose, mwenye umri wa miaka 22,
amekubali kuondoka kwa Luka Modric White Hart Lane na amesema sasa hajui
mustakabali wake katika klabu hiyo chini ya kocha mpya, Andre
Villas-Boas.
KLABU ya Chelsea ipo karibu kumsajili mdogo wake, Eden Hazard,r Thorgan,
mwenye umri wa miaka 19, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa Lens,
Antoine Sibierski.
SUAREZ AWAPIGA VIJEMBE MAN UNITED
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Luis Suarez, ambaye alifungiwa mechi
nane kwa kashfa ya ubaguzi dhidi ya Patrice Evra, amefufua malumbano na
beki huyo Mfaransa wa Manchester United, akitumia Televisheni ya Uruguay
kusema: "Kwa England, Man United wana nguvu ya kisiasa, na unatakiwa
kuheshimu hilo na kufunga mdomo wao."
MSHAMBULIAJI Peter Odemwingie anaweza kuondoka West Brom baada ya kutofautiana na kocha mpya Steve Clarke mazoezini.
KLABU ya Arsenal bado haijaanza mazungumzo ya kujadili mkataba
mpya na Theo Walcott, licha ya kuwapo tetesin kwamba winga huyo wa
England ataondoka bure msimu ujao.
BEKI mkongwe, David Weir, mwenye umri wa miaka 42, yuko tayari kucheza tena Everton iki3wa atahitajika.
YAYA MPANDA BAISKELI...
MWANASOK bora Afrika, Yaya Toure anafanya mazoezi ya kutumia
baiskeli katika klabu yake, Manchester City kujiandaa na msimu mpya wa
Ligi Kuu wakiwa ziarani Austria.
No comments:
Post a Comment