PICHA ZA UKWELI

video: ITV - Mkanganyiko wa kujadili matukio vs Mwenendo wa kesi Mahakamani: Bungeni

Spika wa bunge Mhe. Anna Makinda amepiga marufuku kusomwa kwa baadhi ya vipengele vinavyohusisha kesi zilizo mahakamani katika taarifa ya kambi ya upinzani kutokana na kukiuka sheria na kanuni za bunge zinazokataza kuingilia uhuru wa mahakama.

Kusoma hotuba nzima (unedited): kubofya hapa "Hotuba ya nzima ya upinzani ya Wizara Kivuli ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Nadhani iko namna wananchi tunachukuliwa mapoyoyo kwa kuambiwa hiki hakiruhusiwi kuzungumzwa au kujadiliwa hata ikiwa kipo mahakamani, alimradi tu mjadala wenyewe hauzungumzii mwenendo wa kesi mahakamani bali matukio.

Inanitatiza kuwa hairuhusiwi kuzungumzia matukio hali inaruhusiwa kuripoti na kuandika habari za kesi mahakamani alimradi habari zenyewe hazina lengo la kupotosha au kwa namna yoyote ile kuathiri kufikiwa kwa maamuzi na kutolewa hukumu.

Ujinga wa jambo ni kitu kibaya, lakini ni kibaya zaidi pale aliyeelimika anapojifanya mjinga au mjinga anapokataa kuelimishwa. Na katika hili la kukataza watu kuzungumzia matukio kwa kisingizio tu cha kuwa jambo hili lipo mahakamani, nadhani ni ujinga.

Nami pia kwa kuwa ni mjinga wa sheria, nawasihi wasomi wa Tanzania waoneshe usomi wao kwa kuuelimisha umma kuhusu masuala haya, huenda nami ujinga wangu utanitoka. Walao najijua ni mjinga lakini aliye tayari kujifunza. Mpumbavu ndiye asiyeaka kujifunza wala kuelimika. Kwake ni upuuzi.

Kwa hili, Nancy Grace ashukuru Mungu na kipindi chake cha CNN wapo Maekani, maana kwetu angeshafungiwa.

Ofkoz, kwetu utaambiwa Nancy Grace huko ni Marekani na hapa ni Dangayika, hatufuati kila kitu wanachofanya wao basi na sisi tufuate, sisi tunachuja na kuchagua... (puke)!

---

No comments: