Kundi la The Chocolate Crew likishangilia kitita cha shilingi milioni
moja mara baada ya kuibuka washindi kati ya makundi saba yaliyojitokeza
kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,ndani ya kiota cha
maraha cha Suncirro,Sinza jijini Dar.Katika shindano hilo kulikuwepo na
ushindani mkubwa lakini mwisho wa siku mshindi ilikuwa ni lazima
ajulikane/apatikane.Shindano hilo ambalo mdhamini wake mkuu ni kampuni
ya bia ya Serengiti ndio mdhamini mkuu wa tamasha kubwa lijalo la Fiesta
linalorajiwa kuanza hapo baadae mara baada ya mwezi mtukufu wa
Ramadhani kuisha.Shindano la namna hii limekwishafanyika katika mkoa wa
Arusha ambapo mshindi lilikuwa kundi la Contegious Crew,mkoani Tanga
kundi la Questions Crew waliibuka washindi pamoja na Viswani Zanzibar
ambapo kundi la B-Six lilishinda.Aidha makundi yote hayo yalijinyakulia
kitita cha shilingi milioni moja.
Mmoja wa majaji na mratibu wa shindano hilo ajulikanae kwa jina la Msami
akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi la The Chocolate
mara baada ya kuibuka kinara jioni ya leo kwenye ukumbi wa Sun
Cirro,sinza jijini Dar.
Baadhi ya mwashabiki wakishangilia
Mmoja wa watangazaji wa Clouds TV,Babu wa Kitaa kupitia kipindi Bibi
Bomba akiwa amepozi na wadau wengine wa Clouds Media Group wakifuatilia
shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012.
Kundi la Mazabe Ndonga likionesha umahiri wa kucheza jukwaani kwenye
shindano la kumsaka mshindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012,ndani ya
kiota cha maraha cha Suncirro,Sinza jijini dar.Katika shindano hilo
yamejitokeza makundi saba ambayo yameshindana vikali katika kumsaka
kinara wao,zawadi katika shindano hilo ambalo mdhamini wake mkuu ni
kampuni ya bia ya Serengi,ni fedha taslimu shilingi Milioni
moja.Mashindano haya yamekwishafanyika katika mkoa wa Arusha ambapo
mshindi lilikuwa kundi la Contegious Crew,Zanzibar likashinda kundi la
B-Six na mkoani Tanga kundi la Questions Crew waliibuka washindi,aidha
makundi yote hayo yalijinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.
Mmoja wa wasanii wa kundi la The Ridder akionesha mbwembwe zake kwa
mashabiki kibao (hawapo pichani) waliofika kwenye shindano hili jioni ya
leo,ambalo lilikuwa na msisimko mkubwa .
Kundi la Tatanisha Dancers likisaka ushindi kwa udi na uvumba.
Baadhi ya washabiki waliojitokeza jioni ya leo kwenye shindano la
kumsaka mshindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012,ndani ya kiota cha
maraha cha Suncirro,Sinza jijini dar
Mmoja wa majaji wa shindano hilo Isakwisha Thomson kutoka Clouds FM
akifafanua jambo,kati ni Msami kutoka THT pamoja na B-Dozen kutoka
Clouds FM,Wote ndio waratibu wa shindano hilo la Serengeti dance la
Fiesta 2012.
Kundi la Manzese Crew likisaka ushindi kwa udi na uvumba jukwaani kuwania kitita sh milioni moja.
Mashabiki wakifuatilia shindani hilo jioni ya leo.
Kundi la Chocolate lionesha mbwembwe zake jukwaani kuwani kitita cha shilingi milioni moja.
Mmoja wa majaji katika mashindano hayo Isakwisa Thomson akielezea jambo wakati shindano likiendelea.
Mc wa shindano zima,Nickson akiwayataja makundi yaliyotinga fainali
kwenye mchakato wa kulipata kundi kinara la Serengeti dance la Fiesta
2012.
Majaji wakijadiliana jambo kumpata mshindi
Palikuwa hapatoshi jioni ya leo ndani ya ukumbi wa maraha wa Sun Cirro,Sinza jijini Dar.
No comments:
Post a Comment