PICHA ZA UKWELI

Tigo yachangia milioni 26 za madawati katika taasisi ya Hassan Maajar Trust


Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Holiday Inn wakati alipopokea Hundi ya kiasi cha Shilingi milioni 26 kutoka kampuni ya Tigo kwa ajili ya kuchangia Madawati katika Shule za Msingi 5 kutoka wilaya mbili  Njombe na Makete zilizopo mkoani Iringa ambapo alisema kuwa shule zitakazo faidika ni Maendeleo watapata madawati 135, Umoja 196, Kumbila 200, Makonde 152 na Mbela 37. Aliongeza kuwa shule hizo zimechaguliwa kulingana  na kuwepo kwa haja kubwa zaidi ya Madawati  katika picha wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja mkuu  wa Tigo Bw, Andrew Hadgson watatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya kupekea michango ya kusaidia katika sekta ya Elimu Hassan Maajar Trust  Zena Tenga wane kwenda kulia ni Mwenyekiti wa kamati madawati Balozi Betha Somi wamwisho ni Dkt, Sinare Yusuf Sinare Mwenyekiti wa kamati wa ukusanyaji Fedha taasisi ya Hassan Maajar Trust
Mkurugenzi wa taasisi ya kupokea michango ya kusaidia katika sekta ya Elimu Hassan Maajar Trust  Zena Tenga ( katikati)wakiteta jambo na Mwenyekiti wa kamati ya madawati Balozi Betha Somi (kushoto)  na kulia ni  Dkt, Sinare Yusuf Sinare.
Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa akipokea mfano hundi ya Shilingi milioni 26 kutoka kwa Dkt, Sinare Yusuf Sinare Mwenyekiti wa kamati wa ukusanyaji Fedha taasisi ya Hassan Maajar Trust  iliyotolewa na Kampuni ya Tigo ambapo fedha hizo zilipatikana katika mfuko wa matembezi ya Hiyari  ya Tigo tuchange kwa Hassan Maajar Trust.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo jana

No comments: