NDITI MTANZANIA AMBAYE AMEBAHATIKA KUMWAGA WINO CHELSEA
Mchezaji wa Tanzania Adam Nditi jana
amesaini mkataba ‘rasmi’ kama mchezaji wa kulipwa wa klabu ya soka ya Chelsea
ya Uingereza.
Kupitia Twitter jana ameandika; “Leo ni
siku muhimu na ya kukumbuka kwangu na familia yangu na ningependa kumshukuru
Mungu kwa kila kitu nilichonacho na vile navyokuwa.”
“Kuna wakati nakumbuka nilichoka
kimwili na kiakili lakini baada masaa kadhaa ya mazoezi , kujituma na kufanya
kazi kwa biddi naweza kusema hatimaye ndoto yangu imetimia.”
“I'd
like to say well done to @Anditi3 for signing his pro contract with chelsea
today! Official chelsea player! Well done bro! #cfc” alipongezwa na miongoni mwa wachezaji aliokuwa
nao Chelsea Academy aitwaye Dom Solanke.
Adam alijiunga na Chelsea Academy mwaka
2008.
Alicheza kwa mara ya kwanza msimu wa
2010-11 dhidi ya Tottenham Hotspur.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa timu
ya vijana ya Chelsea iliyoshinda kombe la FA mwaka 2011-12 na mara zote alikuwa
akiingia kipindi cha kwanza isipokuwa kwenye mechi ya fainali dhidi ya
Blackburn Rovers, ambapo aliingia kipindi cha pili.
Adam Nditi alizaliwa tarehe 18
September 1994 mjini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment