PICHA ZA UKWELI

Malaika huyu anaomba umchangie nauli kutoka Mwanza afike KCMC akatibiwe moyo

Jina lake ni Yvona Kamugisha (10) binti wa Julius Kamugisha (32), mkazi wa Kirumba wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.

Anaomba msaada wa fedha toka kwa wasamaria wema kote nchini kwa ajili ya nauli na chakula ili apelekwe katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu zaidi ya moyo.

Mwaka 2008 baada ya kupelekwa Hospitali ya KCMC na kugundulika kuwa na tatizo la kupanuka kwa moyo wake, alifanyiwa operesheni na kisha kuruhusiwa baada ya ahueni ya matibabu.

Lakini sasa, baada ya Yvona kupata vipimo vya wataalamu kutoka nchini India waliokuwa katika Hospitali ya Hindu iliyopo mtaa wa Nyakahoja barabara ya Balewa jijini Mwanza, wataalamu wamebaini kujirudia kwa tatizo hilo.

Kwa yeyote atakayeguswa kusaidia, tafadhali wasiliana na baba wa binti Yvona kupitia nambari za simu zifuatazo 0754 724278 au 0782 946177.

via blogu ya Albert G. Sengo

Source: http://www.wavuti.com

No comments: