PICHA ZA UKWELI

Madaktari waliopo mafunzoni “Interns” Bugando waamriwa kurudi Wizarani

Nakala ya amri iliyotolewa kupitia barua iliyobandikwa katika mbao za matangazo katika hospitali ya Bugando inayohitimishwa kwa saini ya Dkt. Majinge, Mkurugenzi Mkuu linasomeka ifuatavyo:



KWA INTERNS WOTE

BUGANDO EDICAL CENTER

Interns wote ambao wamekataa kurejea kazini mpaka jana, wamejisimamisha kuendelea na internship hapa Bugando na mnatakiwa kurudi Wizara ya Afya, hivyo:-

Mnatakiwa kufika Utawla kuchukua barua zenu za kupeleka Wizara ya Afya kwa Msajli wa Baraza la Madaktari na mnatakiwa kuchukua posho zenu za mwezi Juni, 2012 kuanzia saa 2:00 asubuhi tarehe 18/06/2012.

Orodha ya majina imeambatanishwa.

Nategemea ushirikiano wenu.

Dr. Charles R. Majinge

MKURUGENZI MKUU

No comments: