PICHA ZA UKWELI

OFFICIAL: JORDI AITOSA MAN UNITED - KUJIUNGA NA BARCELONA WIKI IJAYO-SHAFFIH


Barcelona wametangaza kwenye mtandao wao rasmi kwamba wamekubalina na Valencia juu ya ada ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Spain Jordi Alba.

Barca ambao wamekuwa wakihusishwa na beki huyo wa kushoto kwa muda mrefu sasa, wamepiga hatua kubwa kuelekea kukamilisha dili hilo lenye thamani ya ‹€14 million.

Alba atakwenda Barcelona kufanya vipimo wiki ijayo, na kusaini dili la mkataba wa miaka 5 mara tu atakapofaulu vipimo vya afya.

"Barcelona wametangaza kwamba makubaliano rasmi yamefikiwa juu ya ada ya uhamisho wa Jordi Alba, kilichobaki ni vipimo vya afya ambavyo mchezaji huyo atafanyiwa wiki ijayo jijini Barcelona." Uliandika mtandao huo wa Barca.

"Gharama za uhamisho huu ni €14million na mchezaji atasaini mkataba wa miaka 5."

Alba mwenye miaka 25 ni zao la chuo cha soka cha Barcelona La Masia, lakini alifeli kufanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza pale Nou Camp na akaondoka mwaka 2005.

Jordi Alba alipokuwa La Masia

Sasa atarudi nyumbani alipolelelewa baada ya kucheza kwenye vilabu vya Cornella, Gimnastic na Valencia.

Habari hii ya Jordi Alba kwa vyoyote itakuwa sio nzuri kwa Manchester United ambao wamekuwa wakihusishwa kumtaka mhispania huyo ili aje ambadili Patrice Evra ambaye umri unamtupa mkono.

No comments: