PICHA ZA UKWELI

USIKILIZE HAPA WIMBO MPYA ALIOUTOA HUYU MWANAFUNZI ALIEANDIKA BONGOFLEVA KWENYE MTIHANI WA FORM IV.


Anaitwa Julius lakini jina lake la kisanii ni ELINAJA.
Kama ulipitwa na hii stori ni kwamba huyu ndio mwanafunzi ambae kwenye mtihani wa kumaliza Form IV aliamua kuandika mistari ya bongofleva badala ya kufanya mtihani kama inavyotakiwa, wiki iliyopita ndio amejitokeza na kutaja sababu tano zilizomfanya afanye hivyo ikiwamo kujitetea kwamba alifanya hivyo kuwakomboa wengine ambao wameshindwa kusema, mfumo wa elimu ni mbovu na haumruhusu mtu asieweza kusoma kufanya kitu cha kipaji chake.
Anavyosema ni kwamba ana kipaji cha muziki lakini Elimu ya Tanzania hairuhusu kukuza vipaji kama chake mashuleni, yani kuna system moja ya elimu ambayo kila mwanafunzi ni lazima aifate… kipaji alichosema anacho ni muziki, isikilize hiyo single yake mpya hapo chini alafu utoa maoni yao umeonaje kipaji chake.

No comments: