Wizara
imepokea malalamiko kuwa kati ya tarehe 23 juni, 2012 hadi tarehe 29
juni, 2012, Madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo 372 kati ya 763
katika hospitali mbalimbali nchini, waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa
ikiwa ni wajibu wao kama madaktari.
Kitendo
hicho sio tu kilihatarisha usalama wa wagonjwa waliohitaji huduma za
matibabu katika hospitali hizo, bali kilikuwa ni ukiukwaji wa maadili ya
taaluma.
Madaktari
hao waliogoma walirejeshwa Wizarani kwa barua kutoka kwenye mamlaka za
hospitali walikokuwa wakifanyia mafunzo kwa vitendo.
Kwa
kuwa Wizara ndio yenye dhamana ya usimamizi wa huduma za afya nchini,
na kwa kuwa madaktari hao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari
Tanganyika, hivyo Wizara imewasilisha malalamiko haya huko ili Baraza
liwachunguze na kuamua hatma yao kitaaluma.
Kwa
hivi sasa madaktari hao hawako maeneo yao ya kazi, na suala hili
limepelekwa Baraza la Madaktari kwa uchunguzi kuhusu kitendo
walichokifanya, hivyo Wizara inasitisha posho zao kuanzia Tarehe 1
Julai, 2012 hadi hapo itakapopata taarifa ya uchunguzi wa Baraza la
Madaktari.
Madaktari
wengine waliogoma, taratibu za kiutumishi zitachukuliwa na mamlaka ya
ajira zao kwa mujibu wa sheria na taratibu husika.
Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
No comments:
Post a Comment