Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya mwandsihi wa mtandao huo, kutaka kujua ni mafanikio gani aliyoyapata baada ya kibao hicho ambacho kwa namna moja amna nyingine ndicho kilichomfanya aweze kujulikana.
Dimpoz stejini
Alisema kuwa mafanikio makubwa ni kwamba kimemfanya aweze kuishi kivyake na kujitengemea kwa kila kitu, kwani awali alikuwa akiishi nyumbani.
Hata hivyo alisema kuwa mbali na mafanikio hayo lakini kimeweza kumpatia mkataba mkubwa na vituo hivyo vikubwa vya muziki Afrika kwani kwa sasa kibao hicho kinapigwa mara zote kwenye televisheni hizo.
“Nahitaji kufika mbali zaidi katika muziki wangu hivyo nafarajika kuona wimbo wangu unapigwa kwenye televisheni hizo, kwani huo ni mwanzo mzuri wa mimi kuonekana kimataifa zaidi,” alisema Dimpoz kwa pozi.
No comments:
Post a Comment