Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya story fupi zilizopigwa na mwandishi wa mtandao huo, ambaye alitaka kujua ni kitu gani alichojifunza kutoka kwa Obama.
Linah katika pozi.
Linah KatikaAlidai kuwa kikubwa ni namna ya kuishi na watu vizuri, kwani angekuwa ni mtukutu wa kujifanya mjuaji basi asingeweza kukaa kwa muda mrefu, na kufanya kazi ambayo kila mmoja aliipenda kutoka moyoni.
“Unapokuwa kwa watu ni lazima utulie na sidhani kama ningekuwa na mambo ya kujifanya najua sana kama ningedumu kwa kipindi chote nilichokaa, lakini kuna mambo mengi ambayo nimejifunza juu ya maisha na muziki wangu kwa ujumla,” alisema ndenge mnana.
Anaongeza kuwa anaamini muziki wake kwa upande fulani umefika kwenye kiwango ambacho kinaweza kumsaidia kimataifa kwani ameweza kutangaza jina lake kwa Obama, ambako ni sehemu nzuri katika soko la muziki kwa wasanii.
“Wasanii wengi wanatamani kufanya muziki Marekani kwani ndiko kwenye wasanii wengi wakubwa, si dhani kama kuna mtu anayebisha juu ya hilo, ingawa zipo nchi nyingi ambazo zinafanya muziki lakini kwa Obama kuko juu,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment