Wasanii hao wa Bongo Movie wakiombewa katika uwanja wa Samora na mchungaji Kikoti jana
TIMU NZIMA YA BONGO MOVIE IKIONGOZWA NA STEVE NYERERE MC
Wasanii nguli wa maigizo na Filam nchini Tanzania kupitia kundi la Bongo Movies wakiongozwa na mwenyekiti wao JB wamerudishwa katika mstari wa kuanza kumtumikia Mungu na kuachana na mambo ya dunia baada ya msanii wa kundi la Orijino Komedy Emmanul Mgaya ama Masanja Mkandamizaji kuwakusanya pamoja na kuwafanyia maombi maalum katika tamasha lake la uzinduzi wa albam ya nyimbo za injili ya Hakuna jipya chini ya jua .
Huku Msanii Jackiline Wolper , Uwoya ,Rich Rich na Cathy wakiushangaza umati wa waumini wa madhehebu mbali mbali na meza kuu chini ya mgeni rasmi naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mhe.Philp Malugu baada ya kutangaza kuokoka huku baadhi yao wakidai bado wapo wapo kwanza.
Msanii Jackline Wolper alionekana kama kivutio kwa wengi katika uwanja huo wa Samora mjini Iringa jana na hivyo baada ya kupewa kipaza sauti (MIC) na MC wa sherehe hiyo Steven Nyerere kwa ajili ya kueleza kama amekubali kuokoka ama lah alijibu kwa sauti kuwa ameokoka kupitia tamasha hilo na kuanza kuchenza muziki wa dini unaokwenda kwa wema wa Mungu umenizunguka
No comments:
Post a Comment