PICHA ZA UKWELI

Marehemu Patrick Mutesa Mafisango.
Na Khatimu Naheka
UONGOZI wa Simba umesema umepokea barua kutoka kwa familia ya aliyekuwa kiungo wao, marehemu Patrick Mutesa Mafisango, ikimuweka wazi msimamizi wa mirathi.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kimya cha muda mrefu ambapo Simba ilikuwa inashindwa kuwasilisha haki mbalimbali za marehemu Mafisango zikiwemo fedha za rambirambi kutokana na kutomjua msimamizi wa mali za familia ya mchezaji huyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema familia hiyo ya Mafisango…

Marehemu Patrick Mutesa Mafisango.
Na Khatimu Naheka
UONGOZI wa Simba umesema umepokea barua kutoka kwa familia ya aliyekuwa kiungo wao, marehemu Patrick Mutesa Mafisango, ikimuweka wazi msimamizi wa mirathi.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kimya cha muda mrefu ambapo Simba ilikuwa inashindwa kuwasilisha haki mbalimbali za marehemu Mafisango zikiwemo fedha za rambirambi kutokana na kutomjua msimamizi wa mali za familia ya mchezaji huyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema familia hiyo ya Mafisango aliyefariki dunia Mei 17, mwaka huu kwa ajali ya gari, imetuma barua ikimtambulisha Mbuyi Ilemba Orly kuwa ndiye anayetakiwa kupokea chochote kinachomhusu kiungo huyo wa zamani.
Hata hivyo, Kamwaga alisema wameandika barua kwa familia hiyo, wakiitaka itume tena barua yake kupitia kwa ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini ili kujiridhisha zaidi.
“Hivi tunavyoongea, Simba tumepokea barua ambayo inajieleza imetoka katika familia ya marehemu Mafisango, ikimtaja mtu anayeitwa Mbuyi Ilemba Orly kuwa ndiye msimamizi wa haki zozote za marehemu.
“Sasa sisi kama Simba tumeona kuna haja ya kujiridhisha zaidi. Ili kujiridhisha, tumeiandikia barua familia hiyo, tukiitaka itujulishe hilo kwa kuipitisha barua hiyo kwenye ubalozi wa Congo.
“Tumefanya hivyo ili sisi kama Simba tusiweze kuingia katika matatizo yoyote, kwa sababu inawezekana kukawa na wajanja wamejiandikia barua hiyo ili

No comments: