PICHA ZA UKWELI

Cecafa yavuruga kuhusu Yondani

Kelvin Yondani.
Na Mwandishi Wetu
MAMBO yanaonekana kutotulia kuhusiana na beki Kelvin Yondani iwapo ataichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 14 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kanuni za Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), zinasisitiza lazima mchezaji awe na leseni aliyoitumia katika ligi kuu ya nchi yake au iliyoidhinishwa na shirikisho lake.
Yondani ana leseni ya Simba kwa kuwa ndiyo aliyoitumikia…
Kelvin Yondani.
Na Mwandishi Wetu
MAMBO yanaonekana kutotulia kuhusiana na beki Kelvin Yondani iwapo ataichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 14 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kanuni za Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), zinasisitiza lazima mchezaji awe na leseni aliyoitumia katika ligi kuu ya nchi yake au iliyoidhinishwa na shirikisho lake.
Yondani ana leseni ya Simba kwa kuwa ndiyo aliyoitumikia msimu uliopita, kuhusiana na Yanga, bado TFF haijamuidhinisha kwa kuwa Simba inasisitiza ni mchezaji wake na imeshawasilisha mkataba katika shirikisho hilo.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, amesisitiza utaratibu kufuatwa kabla ya mchezaji yeyote kuanza kuitumikia klabu katika Kagame.
“Lazima kila mchezaji awe na leseni katika Kagame, iwe imeidhinishwa na shirikisho lake. Tusingependa kuona kuna malumbano baada ya kuanza kwa michuano.
“Kama kuna mchezaji mgeni, basi klabu zihakikishe zimemalizana na taratibu zote zimefuatwa,” alisema Musonye.
Kwa Yondani, TFF italazimika kulimaliza suala lake ikiwezekana kwa kuzikutanisha klabu hizo au kufuata taratibu kwa kuangalia mikataba na kama ule wa Simba utakuwa ni halali, basi itakuwa vigumu beki huyo kuitumikia Yanga katika Kagame.
Wakati huohuo, TFF imezionya klabu za Tanzania Bara kwa kuzitaka zitumie wachezaji waliosajiliwa tu, ambao watashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, amezitaka klabu za Yanga, Simba na Azam zinazoshiriki michuano hiyo, kuhakikisha haziitumii vibaya michuano ya Kagame kwa kuwajaribu wachezaji kabla ya kuwasajili.
“Tunazitaka klabu shiriki za Simba, Yanga na Azam kutotumia michuano hii kwa ajili ya kuangalia wachezaji kabla ya kuwasajili.
“Zihakikishe kuwa wachezaji zitakaowatumia ni wale ambao tayari zimewasajili kwa ajili ya kuwatumia kwenye ligi,” alisema Osiah.
Mohammed ‘Meddie’ Kagere na Yondani ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Yanga hivi karibuni na majina yao bado hayajapitishwa na TFF, wakati Patrick Nkanu, Lino Musombo ni kati ya nyota waliotua Msimbazi wiki kadhaa zilizopita.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi, ndiyo watakaofungua pazia la michuano ya Kagame kwa upande wa timu za Tanzania, kwa kuivaa Atletico ya Burundi

No comments: