Release No. 119
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 16, 2012
CRDB YASHINDA TENDA YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Benki ya CRDB PLC imeibuka mshindi wa tenda ya kutengeneza tiketi za
elektroniki za kuingilia uwanjani iliyotangazwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF).
Kampuni saba zilijitokeza katika hatua ya awali ya kuonesha nia
(Expression of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ambapo Aprili 19 mwaka
huu Kamati ya Mipango na…
Release No. 119
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 16, 2012
CRDB YASHINDA TENDA YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Benki ya CRDB PLC imeibuka mshindi wa tenda ya kutengeneza tiketi za
elektroniki za kuingilia uwanjani iliyotangazwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF).
Kampuni saba zilijitokeza katika hatua ya awali ya kuonesha nia
(Expression of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ambapo Aprili 19 mwaka
huu Kamati ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya
shirikisho ilipitia maombi hayo na kupitisha nne kati ya hizo.
Baadaye kampuni hizo nne; CRDB Bank PLC, Prime Time Promotions,
Punchlines (T) Limited na SKIDATA People Access Inc. zilitakiwa
kuwasilisha rasmi tenda zao zikionesha jinsi zitakavyofanya shughuli
hiyo pamoja na gharama ya utengenezaji kwa tiketi moja.
Bodi ya Tenda ya TFF ilikutana Julai 13 mwaka huu kwa ajili ya
kupitia tenda hizo ambapo kampuni zote nne zilifanya uwasilishaji
(presentation) wa jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo, na baadaye kuipa
kazi hiyo benki ya CRDB.
Uamuzi huo wa Bodi ya Tenda uliwasilishwa mbele ya Kamati ya Utendaji
ya TFF. Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake kilichofanyika
Julai 14 mwaka huu iliridhia uteuzi huo wa benki ya CRDB.
Baadhi ya vigezo ambavyo Bodi ya Tenda ya TFF iliangalia na kuipa
CRDB tenda ni uwezo wa kufanya kazi hiyo (capacity), hadhi yake mbele ya
jamii (credibility) katika shughuli inazofanya na teknolojia ya kisasa
itakayotumika kutengeneza tiketi hizo.
Uamuzi wa TFF kutangaza tenda hizo ulilenga kuimarisha udhibiti wa
mapato ya milangoni na kurahisisha mtiririko mzima wa washabiki kupata
tiketi na kuingia viwanjani.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema: “Hatua hii ni muhimu sana, kwani
tulikuwa tukiisubiri kwa muda mrefu. Si tu itaimarisha udhibiti wa
mapato, bali pia itaondoa matatizo ya tiketi na kuendelea kujenga
credibility (kuaminika) ya TFF. Mafanikio haya si kwa TFF pekee bali
mpira wa miguu kwa ujumla.”
CRDB imeanza mara moja mchakato wa shughuli hiyo ambapo tiketi hizo
zinatarajia kuanza kutumika rasmi katika kipindi cha kati ya miezi
miwili na mitatu kuanzia sasa.
Boniface Wambura Mgoyo
ofisa habari
No comments:
Post a Comment