PICHA ZA UKWELI

audio: Dkt. Ndugulile akijieleza Bungeni na kisha kutolewa; Halima Mdee akipewa onyo

 
Audio hii ni ya maelezo ya Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni aliyoyatoa katika kikao cha Bunge jioni hii.

Ikiwa hukufuatilia, tafadhali bofya hapa ili kurejea machapisho mawili ya awali.

Baadaye, wakati Naibu Spika, Job Ndugai alipokuwa anazungumza, Halima Mdee (Mbunge wa Kawe) alitaka kutoa taarifa lakini Naibu Spika alimkatalia kutoa taarifa hiyo kwa kusema kuwa Mbunge hapaswi kumpa taarifa Mwenyekiti isipokuwa Mbunge mwenziye na kumtaka aketi chini na kusema anawataka Wananchi wa Kawe kuona jinsi walivyochagua kituko.

Bofya kifute cha pleya kusikiliza...

Baadaye, alipata nafasi Mbunge mwingine (?Wenje ?Lwenje ?Lwenge sina uhakika na jina, samahani) na kuomba mwongozo ambapo alimtaka Naibu Spika, Ndugai aifute kauli aliyoitoa dhidi ya Mdee. Hata na hivyo, Naibu Spika hakufuta kauli yake.

Bofya kifute cha pleya kusikiliza hayo na pia, taarifa ya Lugola iliyofuatia kuhusu tangazo la mnada wa kuuzwa kwa mali na kiwanda cha General Tyre - Arusha, taarifa ambayo ilitolewa maelezo na Jaji Werema.

 



No comments: