Wanafunzi wakiendelea na masomo yao huku wengine wakitumia magoti yao kama sehemu za kuandikia huku wakiwa wamekaa chini.
Uhaba
wa madawati katika shule za msingi na sekondari umeendelea kuumiza
vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini.
Upungufu
wa madawati katika shule za msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha
elimu nchini huku ukichangia kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha
wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na mazingira ya shule kwa
ujumla ambayo si rafiki kwao.
Matokeo
ya wanafunzi kukaa chini husababisha wanafunzi kuandika wakiwa
wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na
hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema.Hali hii
kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.
CHANZO: HAKI ELIMU, TANZANIA. http://hakielimu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment