Nyota  ya jaa ya mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na Uganda Emmanuel Okwi,  inazidi kuwaka, siku chache baada ya klabu bingwa ya Orlando Pirates  kutuma barua ya kutaka mshambuliaji huyo wa Simba aende kufanya  majaribio kwenye klabu hiyo, leo hii timu pinzani ya Orlando kwenye ligi ya Afrika kusini, Mamelodi Sundowns wameuambia uongozi wa Simba kwamba wapo tayari kumnunua mshambuliaji huyo.
Taarifa  zilizothibitishwa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kwamba  Mamelodi wametuma maombi ya kutaka kumsaini Okwi ambaye amekuwa na msimu  mzuri sana ndani na nje ya ligi kuu ya Vodacom msimu ulioisha.
Pia  chanzo changu hicho cha habari kutoka ndani ya Simba kilisema kwamba  kuna timu moja inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A, wameonyesha nia  ya kumtaka Okwi lakini wamesema kwamba wanasubiri mpaka michuano ya Euro  itakapoisha ndipo watakapoamua juu ya suala la usajili wa mshambuliaji  huyo wa kimataifa wa Uganda.

No comments:
Post a Comment