Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Taifa, Mohamed Mpinga, amewataka wananchi kutoa taarifa za madereva wanaokiuka taratibu za usalama wanapokuwa safarini ili waweze kuwachukulia hatua zinazostahili.
Mpinga alitoa kauli hiyo jana mbele ya madereva wa mabasi hayo katika Kituo kikuu cha Mabasi cha Ubungo, wakati wa uzinduzi wa utaratibu mpya wa kuwabana madereva hayo unaofanywa na Jeshi hilo kwa ushirikiano na Benki ya Posta.
Alisema ndani ya utaratibu huo, wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa maofisa wa Usalama Barabarani pale basi wanalokuwa wamepanda linapokiuka sheria za barabarani ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya dereva husika.
“Hivyo nawasihi madereva wote kuwa makini kwa kuepuka kuvunja sheria za usalama barabara kwa ajili ya kulinda usalama wa abiria wenu, pia ili muweze kujiepusha na matatizo yanayoweza kuwapata kwa kukiuka agizo hilo,” alisema Mpinga.
Kupitia utaratibu huo, mwananchi ataweza kutoa taarifa kwa maofisa Usalama Barabarani wa kila mkoa bila malipo, kupitia namba ya simu iliyopo katika ‘stika’ inayobandikwa katika kioo cha nyuma ya basi husika.
Aidha, alisema Polisi watafanya ukaguzi wa kila basi la abiria kila siku kwa lengo la kujiridhisha na utaratibu wa matumizi ya stika hizo na kuongeza kuwa basi lolote litakalokutwa limeondoa stika hizo litachukuliwa hatua za kisheria.
Mpinga alisema kwa kuanza utaratibu huo utaendeshwa kwa mabasi ya Mkoa wa Dar es Salaam na baadaye nchi nzima huku akiwataka wananchi na madereva wote kuunga mkono utekelezaji wa mpango huo.
Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema mpango wa utekelezaji wa utaratibu huo umetumia kiasi cha zaidi ya Sh milioni 30 .
Alisema ingawa wameanza Mkoa wa Dar es Salaam, wanatarajia kusambaza stika hizo kwa mikoa ya Mwanza na Arusha.
---
taarifa via gazeti la HabariLeo

Kamanda Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani akizungumza na mara baada ya kuzindua kampeni ya kuweka vibandiko vyenye namba za simu za vituo mbalimbali ambazo abiria watazitumia kwa ajili ya kutoa taarifa za usalama na matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani. Kampeni hiyo inadhaminiwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB)
No comments:
Post a Comment