Wanafunzi wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani ktk Manispaa Singida
Na: Elisante John Singida.
Julai 30,2012.
MGOMO
Uliondaliwa na CWT nchini, umeleta madhara katika Manispaa Singida,
baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuandamana hadi ofisi ya RC leo.
Kwenye
maandamano hayo, watoto wa shule ya msingi Nyerere, Singidani, Ipembe
na Unyankindi, walitembea kilomita tatu hadi ofisi ya Mkuu Mkoa, huku
barabarani wakiimba ‘tunataka haki zetu, walimu wamegoma, tunataka haki
zetu’.
Baada
ya askari polisi kubaini usalama wa watoto hao upo hatarini,
waliingilia kati na kuongoza maandamano hayo hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Wanafunzi hao zaidi ya 600 walijazana katika uwanja wa mbele, jengo la Mkuu wa Mkoa kuanzia saa tatu hadi saa 4:30 asubuhi.
Hatimaye
Serikali ya Mkoa kupitia katibu wa tume idara ya Utumishi wa walimu
Samweli Ole Saitabau, aliwataka kurudi nyumbani hadi kesho, wakaendelee
na masomo katika shule zao.
No comments:
Post a Comment