IKIWA
ni siku chache tu baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Suleiman Kova, kutangaza kupatikana na kumshikilia raia wa
Kenya, Joshua Gitu Mhindi (31) kutokana na kuhusika kwake na tukio la
kumteka na kumpiga Dkt. Steven Ulimboka, baada ya kuhojiwa na kukiri
mwenyewe kuwa alihusika wakati akitubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Mchungaji Josephat Gwejima wa kanisa hilo lililopo Kawe jijini Dar es
Salaam ameibuka na kukuruka futi mia kuhusu tukio hilo.
Mchungaji Gwejima, ametoa ufafanuzi huo jana mbele ya mamia ya waumini wake wakati wa ibada ya Jumapili asubuhi.
Mchungaji
Gwejima, alisema kuwa jana na juzi, watu wengi wakuwa wakimpigia simu
kutaka ufafanuzi juu ya jambo linalowahusu. Kwamba alipigiwa simu kutoka
ndani na nje ya nchi, kwa hiyo na yeye (Gwejima) ameona alifafanue
jambo hilo kabla ya ibada.
Akasema
kuwa Jeshi la polisi wiki hii lilitoa taarifa kwenye vyombo vya habari
kwamba aliyemteka Dk.Ulimboka amekwenda kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima
kutubu, akawa anamtafuta yeye (Mchungaji Gwajima), lakini akawa
hakumpata na alipomkosa akampata Mchungaji Joseph Marwa na akatubu
kwake.
Gwejima
alisema kuwa alipata taarifa hizo kupitia BBC na vyombo vingine vya
habari. Akasema jambo hilo likawaletea kanisani mambo manne.
Akaongeza
kuwa kwanza, kwa tamaduni za kanisani, mtu akienda kutubu zile taarifa
za toba yake huwa hazitakiwi kutangazwa, na hivyo ikaonekana kuwa katika
Kanisa la Ufufuo, mtu amekwenda kutubu toba na yake ikasambazwa kwenye
vyombo vya habari; jambo ambalo yeye hakulipenda.
Akasema
kuwa jambo la pili, inaonyesha kuwa wachungaji wawili ndio waliokuwa
wanatafutwa, ambao ni yeye (Mchungaji Gwajima) na pia Mchungaji Marwa.
Akasema kuwa vilevile jambo hilo halikumpendeza kwasababu watu wengi
hawakuwa na habari.
Jambo
la tatu, akasema Mchungaji Gwejima kuwa kuna wingu zito la utata kati
ya madaktari na serikali na hivyo taarifa hiyo ikataka kuleta picha kuwa
Kanisa la Ufufuo na Uzima limeandaliwa kuisafisha serikali katika jambo
hilo.
Mchungaji
Gwejima akaongeza kuwa jambo la nne, ni kwamba watu wameshangazwa maana
jambo hili lilikuwa halijawahi kutangazwa kwamba kuna mtu aliyehusika
na kumteka Dk.Ulimboka.
Kutokana na hali hiyo, Mchungaji Gwejima akasema kuwa imembidi atolee ufafanuzi jambo hilo.
“Kwa hiyo nitafafanua, bahati mbaya itawafikia hata watu ambao hawakulengwa,” alisema.
Mchungaji
Gwejima alisema ufafanuzi huo haulengi jamiii nyingine iliyo nje ya
kanisa lake, bali unalenga mchungaji ambaye anataka kufafanulia waumini
wake kuhusu taarifa za mtu ambaye alidaiwa alikwenda kutubu kwa kumteka
Dk.Ulimboka.
Akaongeza
kuwa kati ya Juni 26 au 27, walikuwa kwenye ibada ya kumuombea
Dk.Ulimboka maana ailiona si vyema daktari kutekwa na hivyo wakalaani
kwa pamnoja wale waliomteka na mgomo wa madaktari, pia wakailaani
serikali kwa kuchelewa kulipatia ufafanuzi suala la mgogoro huo (wa
madaktari).
Alisema
kuwa walipomaliza kuomba, kwa mujibu wa walinzi wao, akatokea mtu
ambaye aliomba kuonana na mchungaji kiongozi. Walinzi walisema hawezi
akaonana naye mpaka shida yake awaeleze wao, lakini mtu huyo aliendelea
kusisitiza, lakini hata hivyo walinzi hawakumruhusu na kumweleza kuwa
kama ana shida awaeleze wao.
Walinzi
hao walishikilia msimamo kuwa kama hataki kuwaeleza hatapata nafasi ya
kwenda kumuona, hasa ikizingatiwa kuwa mtu mwenyewe alionekana wa ajabu
ajabu, kichaa si kichaa, mtu mzima si mtu mzima.
Mchungaji
Gwejima akaeleza zaidi kuwa walinzi walibaini huyo mtu si salama kwa
jinsi alivyokuwa. Baadaye mtu huyo akasema ametokea Kenya na kwamba yeye
ni Mkenya, na kwamba alikuwa na mambo mengi ya kumweleza mchungaji,
yakiwemo ya kuwa yeye (huyo mtu) na wenzake wa kikundi fulani walihusika
kumteka Dk.Ulimboka.
Akasema
walinzi waliposikia hivyo, wakajua jambo hilo ni zito. Hata hivyo
hawakuweza kumjulisha yeye (mchungaji kiongozi) kwasababu huwa
wanakutana na watu wengi wa aina hiyo. Baada ya hapo, mtu huyo alianza
kuelezea mambo mengi.
Mchungaji
Gwejima akaendelea kueleza kuwa hata hivyo, walinzi walibaini mambo
mengi, ikiwemo kwamba huenda mtu huyu hana akili timamu, hajui atendalo,
ama mtu huyo ametumwa kwa lengo fulani au anayoyasema yana ukweli
lakini walinzi hawakutaka kumjulisha.
“Nataka
nisahihishe kauli ya kwamba alikuwa anataka kutubu… hapana, alikuwa
anamtafuta mchungaji. Hata hivyo, kama alikuwa anatafuta kutubu, yeye ni
Mkenya (na hivyo) angeenda Kenya, tena kwenye kanisa analosali kama
anatafuta kutubu,” alisema Mchungaji Gwejima.
Hata
hivyo, Mchungaji Gwejima akaeleza zaidi kuwa watu wa Mungu waliookoka
hawana utaratibu wa kwenda kumuona mchungaji kutubu, utaratubu wa neno
la Mungu likiwa linahubiriwa, unamuomba Mungu wewe mwenyewe na Mungu
anakusikia.
“Ni
kanisa katoliki pekee ambalo lina utaratibu wa kwenda kumweleza Padre
au Paroko na kumweleza matatizo yako na kuyatubu, lakini makanisa yote
ya Mungu yaliyookoka hayana utaratibu huo,” alisema.
Mchungaji Gwejima alisema kuwa mambo kadhaa yanayoweza kujitokeza katika suala hilo ni kwamba:
-Kwanza,
inawezekana mtu huyo alitumwa hapo ili atokee katika kanisa hilo ambalo
lina maelfu ya watu na hivyo jambo hilo liweze kusikika haraka.
- Pili, inawezekana mtu huyo ni mhalifu anayetembea hapa na pale kufanya uhalifu.
-
Tatu, inawezekana ni kweli mtu huyo ameyatenda anaysema, lakini swali
linakuja ni kama kweli ametenda hayo, kwanini aendelee kuwepo hapa
nchini hadi sasa? Na kwanini aende kusema suala hilo katika kanisa la
Ufufuo na Uzima?
Mchungaji
Gwejima akaendelea kueleza kuwa kutokana na utata wa suala hilo,
ilibidi mtu huyo abebwe msobe msobe na kupelekwa katika Kituo cha Polisi
Kawe. Akasema kabla ya kupelekwa huko kituoni, mtu huyo alisema
amepanga chumba karibu na Kituo cha Polisi Kawe na baada ya hapo,
walizni walikwenda naye kwenye gesti hausi hiyo na kuchukua mikoba yake.
Baada
ya kufikishwa kituoni, polisi waliwaeleza walinzi wa Kanisa la Ufufuo
kwamba, kwa kuwa tayari wamekwisha mfikisha polisi, wamuache na hivyo
walinzi wakaishia hapo.
Mchungaji
Gwejima aliendelea kueleza kuwa wiki tatu zilizopita, polisi makao
makuu walipiga simu kanisani hapo kutafuta walinzi waliomkamata Mkenya
huyo, kwani mtu huyo alipopelekwa kituo cha Kawe akaulizwa kama ni kweli
kuna maneno aliyoyasema pale kanisani ambapo alijibu ni kweli, hivyo
polisi wakaamua kumpeleka kituo cha Oysterbay.
Akasema
walinzi Joseph Marwa na Ernest walikwenda polisi ambapo walieleza
kwamba mtu huyo alikwenda kanisani na kueleza jinsi mtu huyo alivyoeleza
ambapo aliitwa mbele ya watu hao ambapo naye alidai kuwa kufahamu kuwa
alikuja kwa ajili ya kumuona Mchungaji kiongozi.
“Kanisa la Ufufuo na Uzima tumekuwa mbele kusema ukweli,” alisema.
AKILI
Mchungaji
Gwejima alisema kuwa mtu huyo, wakati akiendelea kuhojiwa, alipoulizwa
kwanini anasema maneno hayo, alijibu kuwa ana matatizo ya akili na
kwamba mapepo yakimwingia huwa anaropoka maneno hovyo. Mtu huyo alisema
hayo mbele ya polisi, kwamba ana matatizo ya kuropoka hata kama maneno
hayo hayana ukweli. Alipiga magoti mbele ya polisi na walinzi wa kanisa
la Ufufuo kuomba asamehewe kwasababu ana tatizo la kuropoka na kusema
mambo ambayo hata kama hayapo.
Akasema
kutokana na maelezo hayo, polisi na walinzi walianza kujadiliana maneno
hayo, ambapo walinzi walitoa ushauri suala hilo liishie hapo kanisani
kwa sababu amesema ana tatizo la kuropoka. Walikubaliana, na polisi
walikubali.
Akasema
siku mbili baadaye, Kova alitangaza kupitia vyombo vya habari kwamba
kuna mtu wamemkamata, aliyekwenda katika Kanisa la Ufufuo kuonana na
Mchungaji Kiongozi kwa lengo la kutaka kutubu na kwamba alipomkosa
alimkuta mchungaji Marwa na akatubu.
“Jambo hili limenishangaza sana kwasababu polisi na walinzi walikuwa wameshakubaliana suala hilo liishie hapa,” alisema.
Akasema
kuwa hata hivyo, polisi wao wana akili za kipolisi, siyo kama
wachungaji inawezekana pamoja na kwamba mtu huyou alisema hana akili
lakini inawezekana ni janja yake.
Alisema
kuwa anachokilaani ni kitendo cha polisi kutangaza kwenye vyombo vya
habari kuwa mtu huyo alikwenda kutubu katika kanisa la Ufufuo wakati
hakwenda kanisani hapo kutubu bali alikwenda kumtafuta mchungaji
kiongozi. Kwa maana hiyo kanisa lake haliwezi kukubali suala hilo,
akiamini kwamba limekuja kwa lengo la kuvuruga kanisa la Ufufuo.
Aliongeza
kuwa Polisi hawakuwa sahihi kumtangaza mtu aliyedai amekwenda kutubu
kanisani halafu wakamtangaza kwenye vyombo vya habari hali inayoonesha
kana kwamba viongozi wa kanisa hilo hawana maadili.
Alisema
kosa jingine ni la polisi ni kwamba hata kama ni kweli mtu huyo
alikwenda kutubu lakini si haki kumtangaza kwenye vyombo vya habari.
Aliongeza
kuwa kama mtu huyo alimteka au hakumteka Dk.Ulimboka suala hilo
halilihusu kanisa la Ufufuo. Pia akasisitiza kwamba hakwenda kutubu kwao
bali alitaka kumuona mchungaji kumweleza mambo gani au angemdhuru.
Kanisa halina mashiko kwenye jambo hilo.
Alisema
Polisi wamefanya vizuri sana kumkamata kwa sababu hata kama ni kichaa
cha kwanza ni kumkamata na akawashauri kwanza kabla hawamjafanya wampime
akili mtu huyo ili kubaini kama ana akili sawa.
Pia
akakumbushia kuwa katika mgogoro huo wa madaktari na serikali kuna mtu
ambaye ametajwa na jamii anayeitwa Hemed Msangi ambaye uvumi umeenea
kuwa Dk. Ulimboka alimtambua na kwenye Bunge kuna mbunge alielezea jambo
hilo hivyo akaliomba Jeshi la Polisi limkamate Msangi kwani hiyo
itawasaidia kuondoa wingu lililopo nchini badala ya kumng’ng’ania mtu
huyo.
Alisema
mtu anayeshikiliwa ni mdogo sana kulinganisha na alivyotajwa Hemed
Msangi na kwamba kuna watu wanapenda mgogoro huo uendelee kwa sababu
hawana cha kupoteza lakini wao kanisa la Ufufuo wanacho cha kupoteza.
Aliongeza kuwa suala la serikali kuwafutia leseni madaktari halifai wakati imewasomesha kwa miaka sita.
Aidha,
alisema wanaomshauri Rais wapo ambao hawajui namna ya kumshauri na
kwamba yeye anamfahamu sana Mhe. Rais kuwa ana dhamira njema na Tanzania
lakini ana wasiwasi na wanaomshauri kwamba wanamshauri ushauri usiofaa
kwasababu katika hotuba ya Rais aliongea mambo mengi ambapo alisema
wanatuhumiwa katika kumteka Dk.Ulimboka na serikali ni moja wapo hivyo
ni bora serikali isiwe sehemu ya upelelezi wa tukio hilo.
Alitaka
iundwe tume huru ya kuchunguza suala hilo akisema ni vyema isifanywe na
polisi hao hao wanaotuhumiwa ili kuondoa wingu lililopo.
No comments:
Post a Comment