PICHA ZA UKWELI

Askofu Mdegela Sasa Kufikishwa Mahakamani




Askofu wa KKKT Dayosis ya Iringa, Dk  O.Mdegella


Mchungaji Mtatifikolo ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Kampasi ya Iringa amevuliwa uchungaji kwa madai kwamba amepoteza sifa za uchungaji na za kufundisha wachungaji.
Siku yoyote kuanzia Jumatatu ya Julai 23, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Dk Mdegella ataitwa Mahakamani kujibu madai ya kumfukuza bila kufuata utaratibu Mchungaji Lambert Mtatifikolo wa dayosis hiyo.

Taarifa kutoka kwa wakili wa mchungaji huyo, Wakili Alfred Kingwe zitakazokujia kwa kina , zimedai kwamba Askofu Dk Mdegella alianza kutafutwa wiki iliyomaliza leo na maafisa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Iringa ili akabidhiwe hati ya kuitwa mahakamani.

Hata hivyo Askofu Dk Mdegella hakupatikana, lakini taarifa za uhakika kutoka kwa wakili huyo zimedai kwamba atapewa hati hiyo siku yoyote wiki inayoanza leo.
chanzo:http://www.frankleonard.blogspot.com/ 

No comments: