MJADALA wa hotuba ya bajeti ya serikali na ile mbadala
iliyowasilishwa na Kambi ya Upinzani, jana ulitawaliwa na lugha za
kibabe, matusi, kashfa na kejeli, kutoka kwa wabunge wa vyama vya CCM na
CHADEMA, ambapo Naibu Spika, Job Ndugai, aliamru kutolewa nje kwa
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA).
Ndugai jana alitoa amri hiyo baada ya Mnyika kudai kuwa rais ni dhaifu, kauli ambayo alikataa kuifuta hata baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika.
Kabla ya kufukuzwa, awali Mnyika alilazimika kufuta kauli yake ya kuwaita wabunge wenzake machizi, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika, aliyesema kanuni za Bunge zinakataza mbunge kutoa maneno ya kuudhi.
Akichangia hotuba hiyo, Mnyika alisema kuwa bajeti iliyowasilishwa bungeni haitekelezi ilani ya CCM wala mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao wabunge walipitisha.
Alisema kushindwa huko kumetokana na Katiba mbovu iliyopo ambayo inawafanya wabunge wengi kushindwa kutoa maamuzi yanayolenga kuwaokoa Watanzania masikini.
Mnyika alisema umaskini wa Mtanzania na kilio cha maji nchi nzima kimetokana na udhaifu wa rais wa nchi, upuuzi wa CCM na uzembe wa wabunge.
Kilichomponza zaidi Mnyika na alichokataa kukifuta ni pale aliposema:
“Ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu.
“Na yeye ndiye mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia Mpango wa Taifa imepita kwenye baraza aliloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya urais.
Mnyika pia alisema: “Kwa mujibu wa Katiba rais ndiye ambaye anapeleka
bajeti bungeni, waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais
amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti, ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu
mambo ambayo Bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema Bunge
likiikataa bajeti, rais ana mamlaka ya kuvunja Bunge.Ndugai jana alitoa amri hiyo baada ya Mnyika kudai kuwa rais ni dhaifu, kauli ambayo alikataa kuifuta hata baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika.
Kabla ya kufukuzwa, awali Mnyika alilazimika kufuta kauli yake ya kuwaita wabunge wenzake machizi, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika, aliyesema kanuni za Bunge zinakataza mbunge kutoa maneno ya kuudhi.
Akichangia hotuba hiyo, Mnyika alisema kuwa bajeti iliyowasilishwa bungeni haitekelezi ilani ya CCM wala mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao wabunge walipitisha.
Alisema kushindwa huko kumetokana na Katiba mbovu iliyopo ambayo inawafanya wabunge wengi kushindwa kutoa maamuzi yanayolenga kuwaokoa Watanzania masikini.
Mnyika alisema umaskini wa Mtanzania na kilio cha maji nchi nzima kimetokana na udhaifu wa rais wa nchi, upuuzi wa CCM na uzembe wa wabunge.
Kilichomponza zaidi Mnyika na alichokataa kukifuta ni pale aliposema:
“Ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu.
“Na yeye ndiye mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia Mpango wa Taifa imepita kwenye baraza aliloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya urais.
Mnyika alisema Rais Kikwete anapaswa kumuagiza Waziri wa Fedha na Uchumi kuiondoa bajeti irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho.
Kutokana na kauli hiyo ya Mnyika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Willam Lukuvi, alitoa utaratibu na kudai kwa mujibu wa kanuni za Bunge namba 61 Mnyika alitumia maneno ya kuudhi kwa kumwita Rais Kikwete kwa kumtaja jina kuwa ni dhaifu na kusema CCM ni upuuzi.
“Nataka niseme kuwa katika watu ambao nawaheshimu ni Mheshimiwa Mnyika, tena nasema kutoka moyoni lakini kwa hili mdogo wangu umepotoka, kwa mujibu wa kanuni mbunge yeyote haruhusiwi kumtaja mtu yeyote ambaye hayumo humu ndani ya Bunge, maana hawezi kupata nafasi ya kujitetea, hivyo ni vema ukafuta kauli hiyo,” alisema Lukuvi.
Naibu Spika Job Ndugai alikubaliana na hoja ya Lukuvi ya kumtaka Mnyika kufuta kauli yake.
Hata hivyo, Mnyika hakuwa tayari kufuta kauli yake ya kumwita Rais Kikwete dhaifu, hata alipoombwa tena kufanya hivyo na naibu spika.
Kutokana na hali hiyo, Ndugai alitumia kanuni ya 73 (2) (3) ya kumtaka mbunge huyo atoke nje.
“Sasa ndugu wabunge humu ndani tunaendeshwa kwa kanuni na kwa kuwa mimi ni Naibu Spika wa uhakika sasa ni lazima nihakikishe sheria zinafuatwa.
“Kutokana na kanuni ya 73 kifungu cha 2 na 3, kifungu cha 2 kinaeleza mbunge yeyote haruhusiwi kutumia lugha ya kuudhi wala matusi na mbunge akifanya hivyo anatakiwa kufuta kauli yake kwa maelekezo ya Spika kwa kutumia kanuni zilizopo na endapo mbunge huyo atashindwa kufuta kauli hiyo anatakiwa kutolewa nje hadi muda wa shughuli za Bunge uliobaki uishe.
“Kifungu cha tatu kinaelekeza kuwa mbunge ambaye atatakiwa na Spika kutoa uthibitisho kwa jambo ambalo alilisema bungeni na kushindwa kufanya hivyo anaweza kufutiwa vikao vitano mfululizo vya Bunge, sasa kifungu cha 3 nakiacha kutokana na Mheshimiwa Mnyika kushindwa kufuta kauli yake, sasa nawaagiza askari wangu waliopo hapa ndani kumtoa John Mnyika nje ya ukumbi wa Bunge,” alisema Ndugai.
Wenje adai wapinzani wanaonewa
Hata hivyo, kutimuliwa kwa Mnyika kulizua tena zogo na mtafaruku kati ya Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje na Naibu Spika, Job Ndugai.
Wenje alisimama akiomba mwongozo wa Spika kuhusiana na adhabu hiyo, lakini Ndugai alisimama na kumzuia asiendelee kuhoji maamuzi halali ya kiti, na kwamba ni kuvunja kanuni za Bunge.
Ndugai alimlazimisha Wenje kukaa chini, huku akimtishia kumchukulia hatua, lakini mbunge huyo alilalamika kuwa hatendewi haki na ilimpasa Naibu Spika kumsikiliza hadi mwisho wa hoja yake.
“Kulingana na kanuni za Bunge, mbunge anatakiwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na wala hatakiwi kuingia katika ukumbi wowote ndani ya eneo la Bunge kuhudhuria vikao vyovyote vya kamati za Bunge hadi kesho. Sasa Wenje, unachojaribu kufanya ni kukiuka kanuni na nakutaka ukae chini,” alisema Ndugai.
Akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge, Wenje alisema Naibu Spika alitumia nguvu kuzima hoja yake kwa kuwa hakulenga kuzungumzia uamuzi wa kumtimua Mnyika nje ya ukumbi wa Bunge bali namna adhabu hiyo ilivyotekelezwa.
Wenje alidai kuwa, kitendo cha askari wa Bunge kumfukuza Mnyika hadi nje ya viwanja vya Bunge na kumzuia kuzungumza na waandishi wa habari, haikuwa sehemu ya adhabu iliyotolewa na naibu spika.
Lusinde aibuka tena
Hata kabla ya kuibuka kwa tukio hilo, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), alirusha makombora ya kashfa na kejeli kwa wabunge wa upinzani akidai ni waongo.
Lusinde alisema kuwa bajeti kivuli ya upinzani ni ya uongo mtupu na kuhoji ukamanda wa viongozi wa CHADEMA unatoka wapi.
Mbunge huyo alisema viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakiwadanganya watu kuwa wana uchungu na nchi, wakati pembeni wananufaika na mapato yanayotokana na kazi nzuri ya serikali ya CCM.
“Mwenyekiti Mbowe alikataa posho ya sh elfu 80 na gari la serikali, lakini kwa nyuma anarudi na kupokea. Hawa ndio wanaojifanya makanda, wakati hawana mafunzo,” alisema Lusinde.
Mbali na Lusinde, Mbunge wa Mwibara, Kange Lugola alidai kuwa hotuba ya bajeti ya kambi ya upinzani si kivuli bali ni giza tupu, hivyo akashangaa kuona jinsi viongozi wa vyama vya upinzani walivyodiriki kuvaa ujasiri wa kusema uongo hadharani.
Lugola alidai kuwa hakutegemea uongo huo mkubwa kuzushwa na viongozi hao, na kudai kuwa watu hao waombewe na wao ‘washindwe kwa jina la Yesu.”
Juzi usiku, akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mchemba Mwigulu, alimwaga matusi mazito dhidi ya hotuba ya upinzani, akihoji weredi na elimu ya walioiandaa.
Mchemba alifikia hatua ya kuita hotuba hiyo takataka na kufikia hatua ya kutupilia mbali kitabu cha hotuba hiyo. Hata hivyo hakuchukuliwa hatua zozote.
Abwao akerwa na matusi
Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao (CHADEMA), alionesha kukerwa kwake na wingi wa lugha za matusi na kashfa kwa wabunge wa upinzani, akidai kuwa yanalidhalilisha Bunge.
Alisema ni aibu kwa wabunge wa CCM kubeza hoja za wapinzani kwa matusi, wakati hali za Watanzania kiuchumi ni mbaya.
“Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tuachane na matusi na tutambue kuwa sote tuna jukumu la kuwapigania Watanzania ambao wana hali mbaya na si kushabikia vyama kwa matusi. Alisema angetamani kuona wabunge wanaungana linapokuja suala la masilahi ya nchi ili watoto na vizazi vijavyo watambue na kuthamini kazi nzuri iliyofanywa na waliowatangulia.
Alionya kuwa ingawa bajeti itapita kutokana na wingi wa wabunge wa CCM, lakini watambue kuwa watakuwa wamewaangusha wapiga kura wao.
NCCR-Mageuzi yaiponda serikali
Chama cha NCCR-Mageuzi jana kilivunja ukimya baada ya wabunge wake wawili kuishukia serikali kwa kukosa uongozi bora na siasa safi, mambo yaliyochangia ongezeko la umasikini kwa Watanzania.
Aliyeanza kurusha makombora hayo, ni Mwenyekiti wa chama hicho na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia, ambaye alidai, hali mbaya ya kiuchumi iliyopo sasa imechangiwa na ombwe la uongozi bora ambao umekuwa ukiandaa bajeti iliyojikita katika matumizi mengi kuliko kuwekeza katika shughuli za maendeleo.
Mbatia alisema bajeti ya serikali iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, mwenye dhamana ni bajeti iliyojaa matakwimu mengi ambayo hayana maana yoyote kwa Mtanzania ambaye ni maskini.
Kafulila alipuka
Naye Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR - Mageuzi), amesema kuwa serikali iliyopo madarakani imeshindwa kutatua umaskini wa Watanzania kutokana na viongozi kuwa na upeo ndogo wa kufikiri.
Kafulila alisema bajeti iliyowasilishwa ni bajeti ambayo haina malengo ya kumkomboa Mtanzania na haina dhamira ya kweli ya kupunguza umaskini.
Akizungumzia kilimo, Kafulila alidai kuwa serikali imekuwa hodari kwa kuweka mipango ambayo haitekelezeki na ndiyo maana hakuna juhudi za makusudi za kuwawezesha wakulima kupata pembejeo kwa wakati.
Kafulila alidai kuwa serikali imekuwa hodari kwa kuweka mipango ambayo haitekelezeki na ndiyo maana hakuna juhudi za makusudi za kuwawezesha wakulima kupata pembejeo kwa wakati.
Alisema nchi ina ardhi inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa hekta milioni 29 lakini katika miaka 50 ya uhuru serikali imekuwa inashughulikia hekta nne tu, na ili iweze kulima zilizobaki inahitaji miaka 3,625.
Amesema inashangaza zaidi kwa serikali kukazania kukusanya kodi katika mambo ya bia, na kuhoji vipi ikiwa Watanzania wataokoka na kuamua kuacha kunywa bia.
Alisema ili Tanzania iweze kuendelea, lazima ipate viongozi wazuri na wenye upeo mpana wa kufikiri kuhusu masilahi ya taifa na si wale ambao uwezo wao unaishia kuwaza familia zao tu.
Mbunge huyo alienda mbali zaidi na kudai kuwa kitendo cha serikali kuendelea kuomba misaada ni aibu, akidai kuwa hata nchi ambazo hazina amani na ziko vitani haziombi msaada kama ilivyo Tanzania.
Alidai kuwa anashangazwa na tabia ya serikali kuacha kukusanya kodi katika makampuni makubwa kama ya simu na madini, badala yake yanayobanwa ni ya bia na sigara.
Mbunge huyo aliyashambulia baadhi ya makampuni ya simu, akidai kuwa yanaliibia taifa kwa kukwepa kodi ambayo kama ingelipwa, kusingekuwa na hali mbaya ya fedha nchini.
chanzo ni gazeti TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment