PICHA ZA UKWELI

Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na Wizara Kivuli Tanzania


  BARAZA LA MAWAZIRI KIVULI NA MABADILIKO YA WIZARA KIVULI 2012
No.WIZARA KIVULIWIZARA YA SERIKALIKAMATI HUSIKA YA BUNGEWAZIRI KIVULINAIBU WAZIRI
1.OFISI YA WAZIRI MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU-SHERIA NA KATIBA,
-FEDHA ,UCHUMI +MIPANGO
KUB- FREEMAN A.MBOWE
2.
WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU
1.SERA,URATIBU NA BUNGE
2.UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI
3. TAMISEMI--
ELIMU
-TAWALA ZA MIKOA
-do-
DAVID ERNEST SILINDE

-
3.MIUNDOMBINU UJENZI NA UCHUKUZIMIUNDOMBINU SAID ARFIPAULINE GEKUL
4
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS
OFISI YA RAIS
1-UTAWALA BORA
2-MAHUSIANO NA URATIBU
3- MENEJIMENT YA UTUMISHI WA UMMA
-SHERIA NA KATIBA.
-FEDHA NA UCHUMI
PROF. KULIKOYELA KAHIGI

-
5.FEDHA UCHUMI NA MIPANGO WIZARA YA FEDHAFEDHA NA UCHUMI ZITTO KABWECHRISTINA MUGHWAI
6.KATIBA SHERIA NA MUUNGANO KATIBA NA SHERIA+OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANOSHERIA NA KATIBA TUNDU A.LISSU
-
7. MALIASILI,UTALII NA MAZINGIRAMALIASILI NA UTALII+OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA MALIASILI NA MAZINGIRAMCH.PETER MSIGWA
-
8.MAMBO YA NDANI YA NCHI MAMBO YA NDANIMAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA VICENT NYERERE
-
9. MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKIMAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA+ USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI MAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA EZEKIAH D.WENJERAYA IBRAHIM KHAMIS
10.ULINZI NA JKT ULINZI NA JKTMAMBO YA NJE ULINZI NA USALAMA MCH.ISRAEL NATSE
-
11. MAJI,MIFUGO NA UVUVIMAJI NA UMWAGILIAJI+ MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI KILIMO ARDHI NA MAJISYLVESTER M.KASULUMBAYI
SABREENA HAMZA
SUNGURA
12. KAZI,HABARI,UTAMADUNI NA MICHEZOHABARI,VIJANA NA MICHEZO+ KAZI NA AJIRA MAENDELEO YA JAMIIJOSEPH O.MBILINYI CECILIA PARESSO
13. NISHATI NA MADININISHATI NA MADINI NISHATI NA MADINIJOHN MNYIKA
-






14.VIWANDA NA BIASHARA VIWANDA NA BIASHARAVIWANDA NA BIASHARA HIGHNESS KIWIA
-
15. AFYA, JINSIA NA JAMIIAFYA NA USTAWI WA JAMII+MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO -HUDUMA ZA JAMII
-MAENDELEO YA JAMII
DR. GERVAS MBASSA CONCHESTA RWAMLAZA
16. ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIAELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI + SAYANSI TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO -HUDUMA ZA JAMII
-MIUNDOMBINU
SUZAN A.LYIMO JOSHUA NASSARI
17. KILIMO NA USHIRIKAKILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA KILIMO, MIFUGO NA MAJIROSE SUKUM KAMILI
-
18.ARDHI,NYUMBA NA MAKAZI ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZIARDHI, MALIASI NA MAZINGIRA HALIMA MDEE
-

Baraza lililopanguliwa ni la mwaka 2011 na lilikuwa hivi:

KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe alitangaza Baraza la Mawaziri Kivuli likiwa na mawaziri 29 wote kutoka CHADEMA.

Mbowe aliwateua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuwa Waziri Kivuli wa Fedha, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kuwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuwa Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri Kivuli katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), amekuwa Raya Ibrahim Khamis, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji amekuwa Esther Matiko huku naibu wake akiwa Vicent Nyerere.

Said Amour Arfi kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mchungaji Israel Natse kuwa Waziri wa Mahusiano na Uratibu, huku Susan Lyimo akiteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Pauline Gekul a;iteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Leticia Nyerere Waziri wa Ofisi hiyo akishughulikia mazingira ambapo Zitto Kabwe amekuwa Waziri wa Fedha huku naibu wake akiwa Christina Mughwai.

Godbless Lema amekuwa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Tundu Lissu, Katiba na Sheria, Ezekia Wenje akienda Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Joseph Selasini alipewa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Silvester Kasulumbai akiteuliwa kuongoza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Wengine walioteuliwa na wizara zao katika mabano ni Profesa Kulikoyela Kahigi (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Halima Mdee (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Mchungaji Peter Msigwa (Maliasili na Utalii).

Mhandisi Salvatory Machemuli aliongoza Wizara ya Ujenzi, Mhonga Ruhwanya (Wizara ya Uchukuzi), Lucy Owenya (Viwanda na Biashara), Christowaja Mtinda (Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Dk Gervas Mbasa (Afya na Ustawi wa Jamii).

Marehemu Regia Mtema (Kazi na Ajira), Naomi Kaihula (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), Joseph Mbilinyi (Habari,Vijana na Michezo), Mustapha Akunaay (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Meshack Opulukwa (Kilimo, Chakula na Ushirika) na Highness Kiwia amekuwa Waziri Kivuli wa Maji.

No comments: