PICHA ZA UKWELI

KIMENUKA: ALLY MAYAY AONDOLEWA KWENYE UCHAGUZI WA YANGA-SHAFFIR DAUDA


Siku kadhaa baaada ya kuwekea pingamizi la kugombea umakamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, mchezaji wa zamani na mjumbe wa kamati ya utendaji ya uongozi uliojiuzulu wa klabu hiyo, Ally Mayay Tembele leo amepigwa panga katika listi ya wagombea wa umakamu wa raisi.


Kw mujibu wa mmoja ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi wa Yanga, Ally Mayay amepigwa panga hilo baada ya kutotokea wakati wa usikilizwaji wa pingamizi hilo uliofanyika leo, pamoja na kwamba jana lilitolewa tangazo likiwataka wanachama wote waliokuwa wamewekewa pingamizi kufika makao makuu kusikiliza mapingamizi yaliyowekwa dhidi yao.


Tunaendelea kumtafuta Ally Mayay ili tuweze kupata kujua ni hatua gani atachukua baada ya jina lake kukatwa.

No comments: